Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 17 July 2014

PAUNI MILIONI 8 ZAMKIMBIZIA DEMBA BA UTURUKI

Demba Ba sasa kuvaa jesi ya Besiktas ya Uturuki

Usajili mpya na mikataba mipya kwa wachezaji vinara ndio shughuli kuu inayoendelea sasa kabla msimu mpya wa michuano kuanza.
Pamoja na kasheshe zinazomuandama, Suarez sasa yuko Bacelona 100% baada ya kuihama Liverpool, nae Demba Ba tayari amewasili Uturuki anakotarajiwa kukamilisha uhamiaji wake kutoka Chelsea hadi Besiktas kwa gharama ya £8m.
Demba Ba amewahi kuifungia Chelsea angalau mabao 14. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa mika 29 ameyathibitisha hayo katika mtandao wa Twitter akionekana tayari kavalia jesi ya Besi-ktas. "Amesema yaliyobaki ni kukamilisha ukaguzi wa kiafya na kuweka saini mkataba.
Hivyo Chelsea wamejibu kwa kumshawishi Filipe Luis aihame Atletico Madrid ingaje Mbrazil huyo yuko katika safu ya ulinzi.
Msimu uliopita Luis alishiriki mechi zaidi ya 40 na kilele ikawa Atletico kushinda la liga kwa mara ya kwanza tangu 1996 na pia wakafikia fainali ya Champions League.

BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment