Pages

Pages

Pages

Friday 11 July 2014

NEYMAR KUUNGANA NA BRAZIL KUSAKA NAFASI YA TATU DHIDI YA UHOLANZI

<> at Castelao on July 4, 2014 in Fortaleza, Brazil.MSHAMBULIAJI majeruhi, Neymar Jr atahudhuria mechi ya mshindi wa tatu siku ya jumamosi kati ya nchi yake ya Brazil dhidi ya Uholanzi.
 Brazil waliomkosa Neymar katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani na kulala kwa mabao 7-1 watachuana na kikosi cha Louis van Gaal ambao kilitolewa jana kwa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ya Argentina.
 Neymar aliyeibeba Brazil mechi za nyuma alikosekana na kusababisha nchi yake ifanyiwe kitendo cha `Ukatili` na Wajerumani.
 Nyota huyo wa Barcelona alivunjika mfupa wa uti wa mgongo wakati wa mechi ya nusu fainali dhidi ya Colombia nah ii ilitokana na kugongwa kwa goti mgongoni na Juan Zuniga.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment