Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Hussein Mwinyi.
Na Mwandishi wetu
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Hussein Mwinyi anatarajiwa kufungua maonyesho ya kongamano la Majeshi ya Nchikavu Afrika ya Mashariki ambapo zaidi ya wataalamu 300 .
Kongamano hilo ambalo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ndiye mshirika mkuu linatarajiwa kufanyika julai 15 na 16 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo lengo kuu ni kujadili changamoto zinazowakabili.
Mkurugenzi wa kongamano hilo la majeshi ya Nchikavu Afrika ya Mashariki, Tracey Lee Zurcher, alisema kuwa Kutokana na misukosuko ya kisiasa wanayokumbana nayo sasa kwa upande wa uharamia na vikosi vya waasi, serikali hizi zinatakiwa kuongeza kwa kasi uwezo wa ulinzi wa nchi kavu pamoja na uwezo wa misaada ya kibinadamu.
“Nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki zina shauku kubwa ya kujilinda, sio tu kwa kuwa na maarifa bali pia kuwa na zana ili kuimarisha miundombinu ya ulinzi wao,” alisema.
Zurcher alibainisha kwamba makongamano waliyoyafanya yameonyesha kuwa kuna haja ya kuwa na ubora wa hali ya juu kimikakati na kiufundi kwa pamoja katika ngazi za kikanda.
Zurcher alieleza kuwa mbali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kutazamia kununua zana za kivita lakini pia wanajivunia kuyakaribisha majeshi na wawakilishi wa serikali kutoka nchi za Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda na Burundi ambao wataelezea masuala muhimu kuhusu ulinzi kwa upande wa nchi kavu na majini pamoja na usalama kwa ujumla.
Pamoja na mambo mengine Zurcher alisema kuwa wataalamu wa masuala ya kijeshi kutoka nchi za Afrika ya Kusini, Malawi, Ethiopia, Msumbiji, na Zambia pia wamealikwa.
CHANZO MO BLOG
No comments:
Post a Comment