Tabasamu kubwa: Mshambuliaji wa Man City ambaye hajatulia , Alvaro Negredo akicheka wakati alipokuwa anapenda ndege kwenda Dundee.
Imechapishwa Julai 10, 2014, saa 10:40 jioni
KIKOSI cha mabingwa wa England, Manchester City kimekwea pipa kwenda Dundee tayari kuanza ziara yao ya maandalizi ya msimu huko Scottish.
KIKOSI cha mabingwa wa England, Manchester City kimekwea pipa kwenda Dundee tayari kuanza ziara yao ya maandalizi ya msimu huko Scottish.
Katika msafara huo, pia umemjumuisha mshamabiliaji ambaye hajatulia kwa sasa, Alvaro Negredo aliyeonekana kuwa katika morali nzuri.
Kikosi cha Manuel Pellegrini kitacheza Dundee siku ya jumapili kabla ya kusafiri siku inayofuata kwenda Edinburgh kucheza dhidi ya Hearts siku ya ijumaa.
Negredo anayehusishwa kuondoka Etihad, alipigwa picha akipanda ndege binafsi ya Man City, `City Jet` jana jioni, huku naye kipa mpya, Willy Caballero akiwemo katika msafara huo.
Kifaa kipya: Kipa mpya wa Man city, Willy Caballaro pia yumo katika msafara wa klabu hiyo kwenda nchini Scotland kufanya maandalizi ya kabla ya msimu.
Big bosi!: Kocha wa City, Manuel Pelligrin atakuwa na kikosi chake nchini Scotland na baadaye atakwenda America.
Ametulia tuli: Samir Nasri alipanda ndege ya klabu kwenda Scotland.
Kitu hewani: Wachezaji wa City wakiwa katika picha iliyowekwa kwenye mtandao wa Twita wa klabu.
Aleksander Kolarov na Stefan Jovetic wakiwa kwenye ndege.
Ndege ya City ikipaa kuelekea Dundee
Vijana wakiondoka Manchester
CHANZO MPENJA
BLOG
No comments:
Post a Comment