Pages

Pages

Pages

Tuesday 1 July 2014

KUMEKUCHA TENA...BAADA YA MAFUTA, GESI, SASA MAGADI SODA KUANZA KUVUNWA


Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot

MONDULI: BAADA ya rasilimali ya Gas kuanza kuchimbwa mkoani Mtwara na kuinufaisha nchi, sasa neema nyingine tena ya uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha magadi soda imewajia Watanzania.
Neema hiyo inatokana na Tanzania kuwa nchi ya pili kwa uzalishaji mkubwa wa magadi soda duniani yatakayoiingizia nchi Dola za Marekani milioni 300 kwa mwaka sawa na Sh.bilioni 480, fedha hizo zitatokana na mauzo ya zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka.
Tayari utafiti umekamilika na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limewataka wananchi wa Kata ya Engaruka wilayani Monduli mkoani Arusha kitakapojengwa kiwanda hicho kujiandaa.
Akizungumza kwenye mkutano mkuu maalum wa Kijiji cha Engaruka, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa NDC Abel Ngapemba alisema, magadi soda hayo yatavunwa kwa miaka 500 ijayo bila kuisha.
Alisema hadi ifikapo Desemba mwaka huu NDC itakuwa imekamilisha taratibu za namna ya kuanza kuvuna madini hayo bila ya kuathiri mazingira yaliyopo eneo husika.
“Mradi ni wa Serikali umepitia hatua zote zinazohusika ili kujiridhisha kwamba hakuna mazingira yatakayoathirika na ndio maana tupo hapa kuwashirikisha na kuwataka mjiandae kwa kuwekena nyinyi.
“Kwa hiyo kinachofanyika sasa hivi ni kuangalia vyanzo vya maji kwa ajili ya kuleta maji katika eneo hili la mradi ambapo tunaamini maji hayo yatawanufaisha,” alisema Ngapemba.
Alisema kukamilika kwa Kiwanda hicho kunatarajiwa kuajiri zadi ya watu 1,000 watakaokuwa wakifanya kazi kiwandani tu aachilia mbali idara na maeneo mengine ambayo yatahitaji wananchi wa eneo la Engaruka kushiriki.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akizungumza na wananchi hao aliwaambia kwamba kazi yoyote ya maendeleo ya kiuchumi siku zote huwa inahusisha vita.
Alisema Serikali imeona ni vyema kuanza kuzungumza na wananchi kwa kuwapatia elimu ya jinsi ya kujiandaa na kunufaika na ujio wa uwekezaji huo badala ya kukaa pembeni na kujiona kama si mradi wao.
“Kinachowaogopesha jirani zetu ni ukubwa wa mradi kwani tukianza uzalishaji hakuna nchi itakayotufikia ndio maana kelele za kututaka tusifanye mradi huu ni nyingi.
“Na wataalamu wamethibitisha kwamba hapa Engaruka kuna magadi soda mazuri zaidi kuliko yanayopatikana kwingine sas abasi katika mazingira kama hayo jirani yako hawezi kukupenda,” alisema DC Kasunga.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Twalib Mbasha alitumia fursa hiyo kuwaelimisha wananchi wa vijiji vya Engaruka Juu na Engaruka Chini namna wanavyotakiwa kujipanga ili kunufaika na
uwekezaji huo.
“Tumeshakubaliana suala hili katika vikao vya madiwani na suala la kupima ardhi ya kijiji tumeliweka kwenye mpango wetu wa mwaka 2014 na 2015. Lakini pia tunatengeneza sheria ndogo zitakazo tawala mradi huu,” alisema Mbasha.
Katika mkutano huo wakuu wa Idara za Mifugo na Uvuvi, Idara ya Maendeleo ya Jamii, Usalama wa Raia na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji ya Baraza la Madiwa waliwaelezea wananchi jinsi ya kubadilisha shughuli za sasa kwa kuziboresha ili wanufaike na ujio wa watu wengi.

No comments:

Post a Comment