Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 11 July 2014

KUMBE WACHEZAJI WA UHOLANZI WALIGOMA KUPIGA PENATI YA KWANZA, VAN GAAL AKAMPA VLAAR!

article-2686845-1F86C10100000578-637_634x474Kama igizo vile: Mlinda mlango wa Argentina Sergio Romero akiokoa mkwaju wa penati uliopigwa na  Ron Vlaar.
KOCHA wa Uholanzi, Louis van Gaal amekiri kuwa wachezaji wawili waligoma kupiga penati ya kwanza baada ya kufungwa kwa penati na Argentina.
Uholanzi walishindwa kurudia kupiga penati kama walivyofanya katika hatua ya robo fainali dhidi ya Costa Rica baada ya beki wa Aston Villa Ron Vlaar kukosa penati ya kwanza na Wesley Sneijder naye kukosa. 
article-2686845-1F86B98800000578-405_634x518Kipa wa Argentina, Sergio Romero akiokoa penati ya kiungo wa Uholanzi,  Wesley Sneijder.
Argentina walifunga penati zote nne na kufika fainali ya kombe la dunia ambapo watavaana na Ujerumani kwenye dimba la Maracana jumapili ya wiki hii.
 
Baadaye, Van Gaal – ambaye anatarajia kuanza kazi wiki ijayo katika klabu ya Manchester United  - alijitokeza na kusema kuwa wachezaji wawili waligoma kupiga penati ya kwanza, lakini hakufafanua zaidi.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment