Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 11 July 2014

HALIMA MDEE: JIHADHARINI NA MATAPELI

HALIMA
Na Mwandishi wetu
Mbunge wa Kawe jijini Dar es Salaam, Halima Mdee (pichani) amewatahadharisha wananchi juu ya utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wasiojulikana katika mitandao ya kijamii kwa kutumia jina lake kwa kudai kuwa anatoa mikopo bila riba.
siku za hivi karibuni kumekuwapo na matukio ambayo yamekuwa yakiwakuta baadhi ya viongozi wakiwemo Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na Mbuge wa Monduli Edward Lowassa.
kwa mujibu wa Mdee ni kuwa  wakati muhafaka kwa Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi ili kuwabaini matapeli hao na kuwachukulia hatua kali za sheria kwani wamelichafua jina lake kwa kulitumia kutapeli watu.
Alisema wamekuwa wakijitambulisha kama Mdee Community Loan na kutumia jina lake lijulikanalo kama Halima James Mdee na kudai kuwa ofisi zao zipo mtaa wa samora jengo la Jmall chumba no 490.
“Huu ni ujinga unaofanywa na hawa watu wenye lengo la kutuchafua, nawaomba wananchi kuwa makini na jambo hili na wanatumia namba ambazo ni 0753990581 au 0653918679, ieleweke kwamba hakuna kitu kama hicho, sijawahi kutoa mikopo wala kuwa na Kampuni inayojishughulisha na mambo hayo” alisema Mdee
Aidha Mdee ameyaomba makampuni ya simu kuwa makini na kufanya uchunguzi ili kuweza kuwabaini matapeli hao kwani wao ni rahisi kuwafahamu kupitia mitambo yao.

CHANZO MO BLOG

No comments:

Post a Comment