Pages

Pages

Pages

Sunday 27 July 2014

GAZETI LA NEW YORK TIMES LATAKA BANGI IHALALISHWE MAREKANI


Raia wa Marekani
Gazeti kubwa na maarufu nchini Marekani, New York Times, limetaka bangi kuhalalishwa nchini humo.
Katika tahariri yake, gazeti hilo limehusisha marufuku ya dawa hiyo na ile ya utumiaji wa pombe katika miaka ya 20 na 30, likidai kuwa hatua hiyo imeleta madhara makubwa kwa jamii.
Linasema kuwa Bangi haina madhara makubwa ikilinganishwa na pombe na tumbaku na kwamba kukamatwa kwa wanaomiliki dawa hiyo kunawaathiri mno vijana weusi.

Majimbo ya Colorado na Washington tayari yameruhusu uuzaji wa bangi kwa lengo la kujiburudisha.
BBC

No comments:

Post a Comment