Pages

Pages

Pages

Saturday 5 July 2014

BRAZIL WAICHACHAFYA COLOMBIA 2-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI, LAKINI `MBUNGI` WALIYOPIGIWA NI HATARI!

article-2681056-1F65BFA200000578-434_634x422Beki wa Brazil,  David Luiz aliachia shuti kali la mpira wa adhabu na kufunga bao la pili na la ushindi.
ULIKUWA usiku mkubwa kwa Wabrazil wakishuhudia vijana wao wa Samba wakicheza mechi ngumu ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya timu ya Colombia.
Haikuwa rahisi kuwazuia Wabrazil waliokuwa na morali ya kushinda mechi ya leo na kuungana na Ujerumani iliyofuzu nusu fainali kwa kuifunga Ufaransa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza.
Usiku huu kumekuwepo na maendeleo, shukurani kwa bao la mapema la Thiago Silva (dakika ya 7) lililowachanganya Colombia.
Ulikuwa mchezo mkali na wenye kasi kwa dakika zote 90, lakini bao la pili lililofungwa na David Luiz kwa shuti kali la mpira wa adhabu katika dakika ya 68 liliwaamusha Wabrazil kwa mara nyingine tena.
Alikuwa kijana mkali, James Rodriguez aliyeifungia Colombia bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 80, lakini yote kwa yote, Wacolombia ndio `bai bai` tena.
article-2681056-1F65B0BF00000578-404_634x428 Luiz akishangilia baada ya kufunga goli kwa shuti la mpira wa adhabu lililomuacha kipa wa Colombia, David Ospina akiambulia manyoya tu.
article-2681056-1F65B95E00000578-473_634x456David Luiz akimshukuru Mungu wake baada ya kufunga, huku Paulinho akimtazama kwa tabasamu.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment