
Shabiki wa Uholanzi akiwa amevalia jezi yake ya rangi ya machungwa akiigiza namna Van Persie alivyofunga bao la kichwa.
WAKATI Robin van Persie anafunga bao bora la kichwa katika ushindi mkubwa wa mabao 5-1 dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe la dunia, Hispania, hakujua kama amefanya kitu cha ajabu katika mashindano hayo.
Bao hilo la kichwa limekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii hususani Twitter.
Mashabiki wengi wa Uholanzi wakiwa katika bustani zao kwa mapumziko, wanaigiza namna mshambuliaji huyo wa Manchester United alivyopaa juu na kupiga kichwa na kufunga bao la bora zaidi mpaka sasa.

Kidume nacho hichoooo! jamaa akiiga staili ya Van Persie.

Kidume nacho hichoooo! jamaa akiiga staili ya Van Persie.

Anakopi: shabiki akijaribu kuigiza staili ya ufungaji ya Van Persie kwenye mechi dhidi ya Hispania.
Kutazama picha zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment