Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 16 June 2014

VICOBA MERU WAPEWA CHANGAMOTO YA KUFUFUA ZAO LA KAHAWA

Benki za Vijijini katika Wilaya ya Meru(VICOBA)zimetakiwa kuhakikisha kuwa zinajiwekeza zaidi katika kufufua zao la kahawa kwani kwa kufanya hivyo wataweza kuongeza faida na ufanisi katika vikundi vyao 

kwa sasa katika Wilaya hiyo ya Meru bado zao la kahawa halipewi kipaumbele kama yalivyo mazao mengine ingawaje zao hilo lina uwezo mkubwa sana wa kuweza kustawi na kuhimili ardhi.

hayo yameelezwa na Katibu wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Arusha Edward Mgwayi kwa niaba ya Mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Arusha John Palangyo  wakati akizindua rasmi wa mashina ya Vikundi vya VICOBA vilivyopo chini ya jumuiya hiyo ndani ya kata ya kikatiti wilaya ya Meru

Mgwayi alidai kuwa zao la kahawa ni moja ya mazao ambayo yana faida kubwa sana lakini yamesahaulika sana ingawaje kama yangekuwa yanatumika kama mazao ya biashara basi yangeweza kuwakomboa wana kikundi

Alisema, Vikundi mbalimbali kwa sasa ni lazima viamke na vihakikishe kuwa vina uwezo wa kuwekeza katika zao hilo ambalo limesahulika ingawaje ni dhahabu kubwa sana katika wilaya hiyo ya Meru.

"ninyi  hapa Meru mna dhahabu kubwa sana lakini hamjajua jinsi ya kuitumia ni zao la kahawa kwa mfano kama jinsi mlivyo kwenye vikundi basi hivyo hivyo umoja wenu utumike katika kusaidia kufufua zao la kahawa”aliongeza Mgwayi

Pia aliwataka nao wanasiasa kuhakikisha kuwa mbali na kuendeleza siasa zao wanatakiwa kusaidia vikundi kama vile VICOBA ambapo kwa kufanya hivyo kutaweza kuruhusu uchumi wa vijijini kukua tofauti na sasa ambapo siasa zipo ila wananchi wanakabiliwa na matatizo makubwa sana

Kwa upande  wana kikundi hicho cha Mwamimi walisema kuwa wana uwezo mkubwa sana wa kubadilisha hata madhari ya eneo hilo la Kikatiti endapo kama watapata fursa za kuwezeshwa kwa njia mbalimbali

Aidha wanakikundi hao walidai kuwa mpaka sasa wameweza kufikia malengo mbalimbali inagwaje bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kutatuliwa ili kuweza kuruhusu maendeleo ndani ya eneo hilo la kikatiti.

Hataivyo Jumla ya mashina saba yaliweza kuzinduliwa huku jumla ya zaidi ya Milioni tatu nazo zilipatikana kwa ajili ya maendeleo ya kikundi hicho cha Mwamimi.

No comments:

Post a Comment