
Toka nje: Kostas Katsouranis (katikati) alioneshwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi mbili za njano dhidi ya Japan.
WAKATI Luis Suarez akiwafanyia kitu mbaya England jana, mchezo mwingine wa kundi C baina ya Japan na Ugiriki ulimalizika kwa suluhu pacha ya bila kufungana.
Kama ilivyokuwa kwa Uruguay na England, timu hizi mbili ziliingia katika raundi ya pili ya mechi za makundi zikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi za ufunguzi.
Lakini kwa Uruguay mambo yalienda vizuri kufuatia Suarez kufanya kazi nzuri katika mchezo wa jana usiku akifunga mabao 2 katika ushindi wa 2-1.
Matokeo hayo ni mazuri kwa Tembo wa Pwani ya Magharibi mwa Afrika, timu ya taifa ya Ivory Coast, lakini lazima washinde mechi ya mwisho kama wanataka kusonga hatua ya 16.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment