Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 25 June 2014

SERIKALI YA UMOJA IRAQ NI KUVUNJA KATIBA - WAZIRI MKUU

Nouri al Malik
Nouri Al Malik na John Kerry
Waziri mkuu nchin Iraq Nouri al Malik ameonya kwamba kubuni serikali ya umoja nchini humo ni mapinduzi dhidi ya katiba ya taifa hilo,na kuwa itaharibu mfumo wa demokrasia uliwekwa kufuatia kung'atuliwa mamlakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo marehemu Saddam Hussein miaka kumi na moja iliopita.
Marekani na mataifa mengine wamekuwa wakimshinikza waziri huyo mkuu kubuni serikali itakayoshirikisha wote kufuatia uchaguzi mwezio Aprili huku watu wa dhehebu la kisunni walio wachache na wale wa kikurdi wakiwakilishwa.
Nouri Al Malik alikuwa akizungumza katika runinga ya taifa hilo wakati wa hotuba yake ya kila wiki kwa taifa.Hatua hiyo inajiri baada ya wanamgambo wa kisunni ISIS kuteka eneo kubwa la taifa hilo.
Lugha nzito aliyotumia kupinga wazo la serikali ya kitaifa wakati ambapo kuna tishio la wapiganaji wa kisunni ni onyo kubwa.
Bwana malik anaweka wazi kwamba atabuni serikali ya chaguo lake kwa kuwa ana haki kulingana na katiba kufuatia uchaguzi wake wa mwezi Aprili ambapo chama chake kilishinda kwa kura nyingi.

Matamshi yake yanaonyesha uwezekano kwamba serikali yake mpya ambayo nisharti ibuniwe mnamo mwezi Agosti haitakuwa ya uwakilishi kama inavyoshinikizwa na Marekani.
BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment