Taarifa zilizotufikia muda mfupi uliopita zinaeleza kwamba, Rais
wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha CUHAS (Bugando) jijini Mwanza, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi Vyuo Vikuu Tanzania TAHLISO), Mussa Leonard Mdede, ameokotwa
usiku huu akiwa hajitambui na amekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando kwa ajili ya vipimo na matibabu.
Inaelezwa kwamba, Mdede
alitoweka ghafla Jumatano iliyopita (Juni 18, 2014) majira ya saa 10 jioni na haikufahamika mara moja mahali alikokuwa mpaka usiku huu taarifa za
kupatikana kwake zilipotolewa.
Kwa mujibu wa jukwaa la wanabidii, taarifa hizi zimethibitishwa na Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi chuoni hapo, Benjamin Thomas.

No comments:
Post a Comment