Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 12 June 2014

MATUMAINI YA BRAZIL KWA NEYMAR, PELE AWAONYA

Pele; Neymar asiachiwe mzigo pekee yake

Mchezaji wa kitambo wa Brazil ana wasiwasi kuwa taifa hilo linamshinikiza mshambulizi wa Neymar kuisaidia taifa hilo kunyakua taji la Kombe la Dunia kwa wenyeji hao na huenda ikamkosesha mshambulizi huyo machachari wa Barcelona umakini.
Neymar mwenye umri wa miaka 22 hajawahi kushiriki Kombe la Dunia lakini amefunga jumla ya mabao 7 kati ya michuano 9 iliyocheza na kushinda Brazil.
“Ni mzigo mkubwa sana kwake kuachiwa majukumu yote.”“Neymar ni mchanga,” Pele alimwambia Gary Lineker katika mahojiano ya kipindi cha BBC Match of the Day.
Brazil wamewahi kushinda Kombe la Dunia mara tano lakini hawajashinda taji hilo tangu mwaka wa 2002.
Wenyeji hao ambao watachuana na Croatia katika mechi ya kwanza ya mashindano hayo jijini Sao Paulo siku ya Alhamisi, walishinda kombe la Mashirika la mwaka wa 2013 kwa kuwalaza mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Uhispania mabao 3-0 katika fainali.
Neymar ambaye anaichezea Barcelona aligonga vichwa vya habari kwa mchezo wake mzuri katika mechi hiyo na kuifungia Brazil bao la pili kwa mkwaju aliopiga kwa mguu wa kushoto.
Timu hiyo inayoongozwa na Luiz Felipe Scolari pia imeshinda mechi tisa za kirafiki kwa mpigo tangu waliposhindwa na Uswizi mwezi Agosti, huku wakifunga jumla ya mabao 30 na kufungwa 2 tu.
“Kwa mara ya kwanza katika historia, Brazil ina safu nzuri ya ulinzi kuliko safu ya ushambulizi,” alisema Pele mwenye umri wa miaka 73, mfungajibora zaidi wa mabao wa timu yake ya taifa kwa mabao 77.
“Kiungo cha kati kiko sawa.
Wamejipanga sawasawa.

Natumai tutarekebisha kuanzia safu ya kati hadi ya ushambulizi.”
BBC

No comments:

Post a Comment