
Serikali ya Rais Museveni inategemea kipato chake zaidi kutoka mkusanyo wa kodi
Bajeti katika nchi za Jumuiya ya AfrikaMashariki zinatarajiwa kutangazwa. Ni wakati ambapo mizani ya matumizi na mapato ya serikali huanikwa hadharani.
Biashara katika Jumuiya imekuwa mhimili imara wa uchumi wa nchi ya Uganda kukua, licha ya msukosuko katika masoko ya dunia.
Mwaka huu wa fedha, ingawaje, wafadhili waliikatia misaada bajeti - karibu robo.Kiokozi cha Uganda kiuchumi, kwa mujibu wa Rais Yoweri Museveni - ni Kilimo, Viwanda, Huduma, na Tetama - yaani, teknolojia ya taarifa na mawasiliano (ICT).
Katika sekta hizo zote nne, mali huzalishwa na nafasi za kazi hubuniwa. Hivyo bajeti ya mwaka 2014/15 itamakanikia sekta hizo nne.
Katika sekta hizo zote nne, mali huzalishwa na nafasi za kazi hubuniwa. Hivyo bajeti ya mwaka 2014/15 itamakanikia sekta hizo nne.

Uganda ilipitisha sheria kali zaidi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja
Si kwa sababu za kiuchumi, bali za kisheria; Uganda ilipoamua kupitisha sheria kali zaidi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Labda bajeti itaongelea kirefu athari ya kukatwa msaada huo.
Labda bajeti itaongelea kirefu athari ya kukatwa msaada huo.
Faida ndogo, kipato kidogo
Kipato cha serikali zaidi kinatokana na kodi. Zaidi ya thuluthi mbili mwaka huu wa fedha serikali ikitegemea mkusanyo wa kodi, zaidi ya trilioni 8.
Lakini kukazuka tobo la kama $milioni 148, sababu ya baadhi ya makampuni kushindwa kulipa kodi.
Mojawapo ya sababu ni vita vya Sudan Kusini ambavyo vilivuruga biashara na Uganda, iliokuwa karibu $1bn, kila mwezi.
Uchumi haukukua kwa karibu 7%, badala yake ulizidi 5%, hii ikimaanisha faida za makampuni fulani zilikuwa chini hivyo kipato cha serikali kupungua.
Sekta binafsi ambayo inatiliwa shime na serikali pia inatapatapa kutokana na gharama kubwa ya mikopo, kwani kima cha riba ya benki kuu kikoo juu sana, 11%, na kuifanya mikopo katika benki za kibiashara kuwa ghali mno kwa wafanyabiashara wengi wadogowadogo, ambao ni mhimili wa uchumi.
Kupanda kwa gharama ya maisha
Thamani ya shilingi iko chini kulingana na fedha ngumu kama dola, na hivyo kuyafanya maagizo kuwa ghali zaidi, mfano petrol au magari ambayo huagizwa kutoka nje.
Matokeo yake ni nauli kuwa juu na bei za vitu kupanda, japo serikali inasema inadhiiti vyema mfumko wa bei ambao uko kasoro ya 6%.
Ingawaje serikali ya Uganda, inatazamia mafuta kuanza kuuzwa mwaka huu wa fedha, huenda ikaamua kugharamia matumizi yake muhimu si kwa kupandisha zaidi kodi, bali kwa kupata mikopo katika masoko ya fedha ndani na nje ya Uganda.
Kwa mfano, mikopo inachangia kasoro ya 30% ya zao ghafi la ndani Uganda - ni kiwango cha chini, kulinganisha na Kenya 50% na Tanzania40% hivi.
Ingawaje, mfuko wa fedha wa kimataifa, IMF na Benki ya Dunia na wadeni wengine wataiwasa Uganda isiandame mkondo huo wa madeni.
BBC
No comments:
Post a Comment