Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 24 June 2014

KIWANDA KIKUU CHA MAFUTA CHATEKWA IRAQ

Wapiganaji wa Kisunni wamekuwa wakiteka miji nchini Iraq na kuwaacha maelfu bila makao
Wapiganaji wa Kisunni nchini Iraq wameteka kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta nchini humo katika eneo la Baiji Kaskazini mwa Baghdad.
Kiwanda hicho kilikuwa kimezingirwa kwa kipindi cha siku kumi huku vikosi vya serikali vikizuia shambulizi la waasi mara kadhaa.
Msemaji wawaasi hao amesema kuwa kiwanda hicho sasa kitapewa usimamizi wa makabila yanayoishi katika eneo hilo na kwamba mapambano ya kuuteka mji mkuu wa Baghdad yataendelea.
Utekaji nyara wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Baiji ni muhimu sana kwa waasi hao iwapo watasimamia maeneo ambayo wameyateka kufikia sasa, hasa kwa kutoa umeme kwa mji wa Mosul.
Wakati huo huo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry, ameahidi msaada mkubwa kwa jeshi la Iraq wakati wapiganaji wa Kisunni wakiendelea na mashambulizi yao nchini humo.
Alisema Waziri Mkuu, Nouri al-Maliki na viongozi wengine wameahidi kuunda Serikali ya Umoja inayowashirikisha wote ifikapo mwisho wa mwezi.
Kiwanda cha mafuta ambacho kimedhibitiwa na waasi wa kisunni
Daktari Zuhair Al-Naher, msemaji wa Serikali ya Iraq ambaye pia ni mwanachama wa chama tawala cha Waziri Mkuu Nouri al-Maliki, Islamic Dawa Party, anasema kuwa anaamini kuwa Bwana Maliki ataunda Serikali ya kuwashirikisha wote.
Bwana Kerry alikuja Baghdad kwa mambo mawili.
Kwanza kabisa kumshinikiza Waziri Mkuu Nouri al-Maliki na viongozi wengine wa kisiasa kuwa wanapaswa kuwa na Serikali mpya, pana inayofuatia uchaguzi mkuu uliofanywa Aprili. Mamlaka yanapaswa kugawiwa Wasunni na Wakurdi walio wachache na sio kwa Washia ambao ni wengi pekee.

Pili Bwana Kerry alitaka kuhakikishia Serikali ya Iraq kuwa Marekani itasaidia wanajeshi wa taifa hilo wanapendelea kupambana na wapiganaji wa Kiislamu wa kundi la ISIS. BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment