Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA), Sepp Blatter, amesema yuko tayari kuendelea na wadhifa huo kwa muhula mwingine wa 5, hivyo kufikisha miaka 20 tangu alipoingia madarakani mwaka 1998 akichukua mikoba ya Joao Havelange wa Brazil.
Akizungumza katika kikao maalum cha FIFA hukoSao Paulo, Brazil amesema yuko tayari kugombea tena cheo hicho kama rais wa shirikisho hilo kubwa linalosimamia soka ya dunia.
Awali Blatter mwenye umri wa miaka 78 alikuwa amedokeza kuwa angestaafu baada ya kipindi chake cha sasa.Kwa kutangaza hivyo ni kwamba amepuuzilia mbali kauli za maafisa wa soka wa Europawanaomtaka ajiuzulu kufuatia madai ya rushwa yanayoiandama FIFA,wakati ilipochaguliwa Qatar kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia 2022.
Blatter pia amependekeza kuwa mameneja wa timu waruhusiwe kutafuta haki pale kwa kutumia teknolojia pale watakapohisi maamuzi ya refa hayakuwa sawa.
Tisho la Maandamano
Wakati huo huo, watu 10 wameripotiwa kukamatwa na kupelekwa vituo vya polisi hukoRio de Janeiro ili kuhojiwa kuhusiana na kushiriki kwao katika maandamano yenye ghasia.
Ulinzi unaendelea kuimarishwa hasa katika miji ya Sao Paulo na Rio ambako baadhi ya makundi ya watu wametishia kufanya maandamano kudai maslahi yao, wakati wa ufunguzi wa Kombe la Dunia utakaofanyika saa chache kuanzia sasa.

No comments:
Post a Comment