Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 20 May 2014

UNATAKA KUFANIKIWA KATIKA MAISHA? HAKUNA UCHAWI, SIKIA USHUHUDA HUU WA ENOS SALEMA!


Ndugu zangu,
Watu wengi wanataka mafanikio katika maisha. Iwe kwenye biashara au hata taaluma. Hakuna anayependa kubaki alivyo, ndiyo maana leo hii kampuni kubwa kama ya SS Bakhressa bado inatengeneza bidhaa za Shs. 10 tu licha ya kupata mafanikio makubwa barani Afrika.
Matajiri wanataka kuendelea kuongeza kipato, hawataki kushuka. Fukara nao wanataka wajikwamue na maisha waliyonayo. Ukimkuta mtu ameng'ang'ana kwenye umaskini leo hii na kusema 'amezowea shida' ujue huyo ana matatizo, siyo bure.
Wapo wanaofanikiwa kwa njia halali kabisa, lakini pia wapo wanaofanikiwa kwa kutumia njia haramu. Siwezi kumhukumu yeyote kwa sababu Mungu ndiye mwenye jukumu hilo.
Kuna wengine wanaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji kutoa makafara, yakiwemo ya damu pamoja na kupoteza ndugu zao, ili waweze kufanikiwa katika maisha. Wengine wanapewa masharti magumu ya kutoufurahia hata utajiri wanaoupata ikiwemo kuambiwa walale sakafuni, wasivae nguo nzuri, wale chakula cha chukuchuku na mambo mengine kadha wa kadha. Huo ni utumwa wa mali kwa sababu badala ya mali ikutumikie, wewe ndiwe unayeitumikia. Raha ya kujihangaisha kutafuta mali iko wapi ikiwa hata nyama unakatazwa na mganga usile?
Lakini ndugu zangu, tunaweza kuongeza vipato vyetu kwa njia halali kabisa, tena hata Mungu atatubariki, ikiwa tutazingatia mbinu za ujasiriamali na biashara.
Tafadhali, tazama video hii ya Bwana na Bibi Enos Salema, ambao wamefanikiwa vya kutosha kutokana na kuzingatia mbinu za ujasiriamali.
Kama utakuwa umevutiwa nayo, tafadhali nipigie 0656-331974 niwape maelezo zaidi.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Iringa, Tanzania

No comments:

Post a Comment