Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 10 May 2014

UKITAKA ASALI, NJOO MANYONI

Misitu ni uhai, na ukiitumia vyema inaleta neema. Kweli kabisa. Ile tabia ya zamani ya kufyeka misitu imetoweka kabisa katika Mkoa wa Singida, hususan wilaya ya Manyoni, ambapo sasa badala ya kuikata miti ili kuchoma mkaa, wanaitumia miti hiyo hiyo kwa ajili ya ufugaji wa nyuki.
Vijiji vingi hivi sasa vimeweka hifadhi ya misitu ya nyuki mkoani humo na wananchi wengi wameweza kujikomboa na umaskini wa kipato kutokana na ufugaji wa nyuki na uuzaji wa asali kama kijana huyu pichani.
Ukitaka asali ya nyuki wakali utaipata, hata ile ya nyuki wapole (mpunze) inapatikana pia. Tena basi, naambiwa asali inayotoka mkoa wa Singida ina soko kubwa kuliko inayotoka sehemu nyingine nchini.
Faida zake ni nyingi, lakini nawashauri Watanzania wenzangu kutumia asali.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Manyoni - Singida

No comments:

Post a Comment