Pages

Pages

Pages

Wednesday 7 May 2014

TEMBO 8 WAUAWA TARANGIRE, MAJANGILI 25 MBARONI

Mizoga ya tembo kama hawa waliouawa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mwaka 2013 imekuwa jambo la kawaida kukutwa kwenye hifadhi zetu kutokana na vitendo vya ujangili vilivyokithiri nchini.

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

UJANGILI bado unaendelea kushika kasi katika maeneo mbalimbali ya Hifadhi ya Tarangire ambapo jumla ya tembo nane waliuawa kwa kipindi cha Novemba 2013 hadi sasa.

Katika kipindi hicho, jumla ya meno 17  ya tembo nayo yakikamatwa katika oparesheni ambayo inaendelea kufanywa na askari wa hifadhi hiyo huku majangili 25 wakitiwa mbaroni.
Hayo yamesemwa na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Tarangire, Stefano Qolli wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya ujangili ambayo bado inaendelea kuitesa hifadhi hiyo iliopo Arusha.
Stefano alisema kuwa kuuuwa kwa tembo hao kunatokana na watu wanaozaniwa kuwa ni majangili kutoka katika vijiji vya jirani kuwawekea mitego mbalimbali tembo hao ikiwemo maboga yenye sumu ambapo pia hali hiyo imesababisha kupungua kwa idadi hiyo ya Tarangire.
Aidha, alitaja mbinu nyingine ambayo imesababisha jumla ya tembo 8 kuuawa, ni pamoja na kuwategea kwa kutumia kamba.
Mbali na hayo alisema jumla ya meno ya tembo 17 nayo yalikamatwa katika vijiji vinne ambavyo ni Kiteto, Kibao cha Manyara Ranch, Marangw pamoja na Kondoa.
"Kupatikana kwa meno haya ya tembo kunatokana na taarifa tulizopata kupitia kwa raia wema pamoja na askari wa kikosi dhidi ya ujangili lakini pia bado tunaendelea na jitiada mbalimbali za kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika wanafikishwa katika vyombo vya dola," aliongeza mhifadhi huyo.
Kutokana na mauji hayo ya tembo pamoja na meno yake jumla ya majangili 25 walikamatwa kwa kipindi cha Novemba 2013 hadi sasa na wameshachukuliwa hatua mbalimbali za sheria ikiwemo kufikishwa mahakamani ingawaje bado kesi zao zinaendelea.
Aliendelea kwa kusema kuwa majangili hayo ambayo kwa sasa yanashikiliwa na vyombo vya dola yaliweza kukamatwa katika maeneo ya Kondoa, Orng’adida, Kiteto, Vilima Vitatu, Manyara Ranch, Marangw, Minjingu, pamoja na Lokisalale.
Katika hatua nyingine, alisema pamoja na jitihada zinazofanywa za kuwalinda wanyama, hasa Tembo, bado hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa maaskari hivyo basi kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza maaskari ili kupunguza tatizo la mauji ya tembo na wanyama wengine.

No comments:

Post a Comment