Pages

Pages

Pages

Wednesday 7 May 2014

BIDHAA ASILIA NI UTALII MKUBWA KWA TAIFA

 Unataka kipi kati ya bidhaa hizi? Hiki ni chetu.
 Bidhaa mbalimbali za asili.
Ndugu zangu,
Wanasema mdharau kwao ni mtumwa, wengine wanasema asiye na asili hana fasili. Swadakta kabisa. Lazima tujivunie vile vya kwetu. Tena vya asili.
Ni dhahiri kabisa kwamba, wengi wetu tuna utamaduni wa kudharau vitu vyetu vya asili na kupenda vile vya Magharibi. Tunawaiga wazungu.
Lakini ajabu ni kwamba, wazungu hao tunaowaiga, ambao waliwaambia babu zetu kwamba hata utamaduni wetu ni wa kishamba, leo hii wanavichangamkia vitu vyetu vya asili huku sisi tukiendelea kuvipuuza. Huu ni utumwa wa fikra.
Naamini kabisa kwamba, bidhaa hizi za asili ambazo wengi wetu tunazidharau ni utalii mkubwa unaoingiza fedha nyingi za kigeni.
Watalii hawana haja ya kwenda mbugani kutazama simba wala mbega, wanakwenda kwenye kiduka kama kile changu pale Iringa na kujipatia vitu hivi vya asili.
Lakini hata sisi Watanzania tunapaswa kuvienzi vitu vyetu vya asili, ambavyo vinatengenezwa na sisi Watanzania wenyewe, katika ule mukhtadha wa kutoa ajira kwa jamii, hivyo kuongeza kipato kwa familia na taifa kwa ujumla.
Tuvienzi vitu vyetu asilia, inaonyesha utaifa wetu jamani.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Arusha, Tanzania
0656-331974

No comments:

Post a Comment