Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 13 May 2014

SIMBA WASIOFUGIKA CAMEROON WATAJA KIKOSI CHA AWALI CHA WACHEZAJI 28 KOMBE LA DUNIA….SAMUEL ETO`O NDANI

404332_heroaSAMUEL Eto`o ametajwa katika kikosi cha awali cha wachezaji 28 cha timu ya taifa ya Cameroon kwa ajili ya fainali za kombe la dunia mwezi ujao nchini  Brazil.
Kocha Volker Finke amemuita Eto`o na kumfanya nyota huyo wa Chelsea acheze fainali zake za nne za kombe la dunia.
Eto`o alicheza fainali za kwanza za kombe la dunia mwaka 1998, akaja kucheza 2002 na 2010 nchini Afrika kusini, na kama atacheza fainali za mwaka huu basi nyota huyo mwenye miaka 33 atafikia rekodi ya  Rigobert Song  na Jacques Songo, ambao waliichezea Cameroon katika fainali nne za kombe la dunia.
 Eto`o ambaye alitangaza kustaafu soka la kimataifa mwaka jana, lakini akabadilisha maamuzi yake pia anatarajia kufikia rekodi ya mabao ya Roger Milla.
Nyota huyo wa zamani wa Cameroon alifunga mabao 5 katika fainali zote za kombe la dunia alizoichezea nchi yake, lakini Eto`o amefunga mabao mawili tu katika fainali tatu alizocheza.
Kusoma kikosi kizima cha Cameroon bofya www.bkmtata.blogspot.com

CHANZO FULL SHANGWE BLOG

No comments:

Post a Comment