HATIMAYE Klabu ya Manchester United amemteua Louis van Gaal kuwa kocha mkuu mpya kufuatia kufukuzwa kazi kwa David Moyes mwezi uliopita.
Mholanzi huyo amechukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa muda wa Man United, Ryan Giggs aliyeteuliwa kuwa kocha msaidizi.
Frans Hoek na Marcel Bout wajajiunga na Van Gaal kama makocha wasaidizi na mholanzi huyo anakuwa kocha wa kwanza kutoka nje kuiongoza Man United.
Van Gaal ataanza kazi rasmi baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil ambako anaiongoza Uholanzi akiwa kocha mkuu.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL
SHANGWE
No comments:
Post a Comment