Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 22 May 2014

'NJOONI MUWEKEZE MANYARA JAMANI'

DC wa Wilaya ya Katesh, Christine Mndeme

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Katesh

MKUU wa Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, Christina Mndeme amewakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, kujitokeza na kujenga chuo cha uuguzi, ili kufanikisha upatikanaji wa wauguzi wengi nchini.
Akizungumza juzi  na wauguzi wilayani Hanang’ Mndeme alisema kukiwa na chuo cha uuguzi Hanang’ kutaondoa uhaba wa wauguzi na kutasaidia kuhudumiwa kwa wagonjwa wengi.
“Pia kukiwepo na chuo cha uuguzi hapa Hanang’ wauguzi watakuwa wanafanya mafunzo kwa vitendo kwenye hospitali yetu ya Tumaini na kituo cha afya Katesh, hivyo wagonjwa wengi watanufaika na fursa hiyo,” alisema Mndeme. 
Alisema uuguzi ni kada muhimu kulingana na mchango unaotolewa na wauguzi, kwani wagonjwa hutumia wakati mwingi zaidi mikononi mwa wauguzi kuliko wahudumu wengine wa afya.
“Ni kweli kwamba wauguzi wana nafasi kubwa ya kubadilisha afya za wagonjwa na kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ya wauguzi ni nguvu ya mabadiliko na rasilimali muhimu ya afya ni sahihi na muafaka kabisa,” alisema.  
Kwa upande wake, muuguzi wa hospitali ya Tumaini ya wilaya hiyo, Anasia Mariki alisema wanaoiomba Serikali iongeze ajira kwa wauguzi ili waweze kupata wauguzi wa kutosha na kutoa huduma bora zaidi kwa jamii.
Mariki alisema wanaiomba Serikali ifanye marekebisho ya muundo wa utumishi wa mwaka 2009 wa kada ya uuguzi, ili wauguzi wapandishwe madaraja kwa wakati na kuepuka madeni hali inasababisha wakose ari ya kufanya kazi.
“Tunaiomba Serikali itoe kipaumbele kwa suala la posho ya wauguzi wanaofanya kazi zamu ya usiku na posho ya kuwa katika mazingira hatarishi na pia Serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya dawa na vifaa tiba,” alisema.

No comments:

Post a Comment