
Kunywa mvinyo haisaidii afya yako.
Je umekuwa ukibugia
mvinyo ili ili ukusaidie kiafya?
Watafiti
wanadai kuwa mvinyo mwekundu (Red wine) hauna manufaa kama ilivyodhaniwa kuwa
nayo kwa moyo wa binadamu.
Wanasayansi
nchini Italia wamekuwa wakichunguza wenyeji 800 kutoka eneo la Chianti maarufu
kwa unywaji wa mvinyo mwekundu nchini humo na kubaini kuwa mvinyo huo hauna
faida yeyote kama ilivyodhaniwa awali.
Aidha
watafiti hao wamegundua kuwa kirutubisho cha mvinyo huo ''Resveratrol''
hakizuii maradhi ya moyo wala kurefusha maisha ya wale wanayoikunywa mvinyo huo
mwekundu.
Prof Richard Semba
"Hadi kufikia hapa tulipo sifa iliyolimbikiziwa kiungo cha
Resveratrol eti kuwa inafaida kubwa kwa siha ya binadamu si kweli. Hakuna
udhibitisho wa kisayansi unaounga mkono sifa hizo za faida kwa afya"
Kufuatia
ripoti yake Professa Semba wakfu wa wagonjwa wa moyo nchini Uingereza tayari
umeanza kufanya utafiti wake kupata ukweli kuhusu kiungo cha resveratrol.
Utafiti
huo hautakuwa wa kwanza.
Utafiti
umefanywa mara nyingi nchini Ufaransa kujaribu kutanzua kitendawili cha matukio
machache sana ya maradhi ya moyo miongoni mwa wenyeji nchini Ufaransa
ikilinganishwa na mataifa yaliyostawi ilihali asilimia kubwa ya wafaransa ni
waraibu wa vyakula vya kukaangwa kwa mafuta mengi na wanywaji wa mvinyo.
Utafiti
wa awali umekuwa ukiashiria kuwa unywaji huo wa mvinyo mwekundu ulaji wa
chocolate na matunda labda ndiyo huzuia maradhi ya moyo.
Watafiti
waligundua kuwa kiungo cha Resveratrol ndicho kibwagizo katika vyakula hivyo
vyote na hivyo kuipigia debe kuwa ndiyo sababu ya afya nzuri ya wafaransa.
Lakini
Prof Richard Semba, kutoka chuo kikuu cha Johns Hopkins ameshindwa kuthibitisha
hilo.
Aliwaongoza
madaktari watafiti wa maradhi ya moyo kuwachunguza wakongwe 783 kutoka mji wa
Tuscany ambao walitoa maelezo kuhusu siha zao vyakula wanavyokula na kunywa na
hata mkojo ili kufanyiwa utafiti na kwa zaidi ya kipindi cha miaka 9.
Katika
kipindi hicho cha miaka 9 wakongwe 268 walioshiriki katika utafiti huo waliaga
dunia 174 walipata maradhi ya moyo na wengine 34 walipatikana wameathirika na
ugonjwa wa saratani.
Resveratrol
haikuonekana kusaidia katika matukio hayo yote na hivyo kutilia shaka faida
yake mwilini.
Daktari
wa moyo nchini Uingereza Maureen Talbot,anasema licha ya ripoti hiyo wakfu wa
magonjwa ya moyo nchini Uingereza hautabadilisha ushauri wake kwa umma kuwa
watu waendelee kula mboga matunda na nafaka.
CHANZO, BBC
SWAHILI
No comments:
Post a Comment