Pages

Pages

Pages

Friday 2 May 2014

‘MUUNGANO WA TANZANIA MFANO KWA NCHI ZA EAC’


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akitoa hotuba juzi jijini Arusha. Picha na Filbert Rweyemamu.

Arusha. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeelezwa kuwa mfano halisi unaothibitisha uwezekano wa kuanzishwa na kudumu kwa Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC).
Wakuu wa nchi za EAC waliokutana jijini hapa jana waliipongeza Tanzania kwa kuadhimisha miaka 50 ya Muungano huo Aprili 26, mwaka huu na kusema huo ni mfano wa kuigwa kwa ajili ya kusonga mbele katika mikakati yao ya kuunda shirikisho la EAC. Akizungumza wakati wa mkutano huo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alisema kama Tanganyika na Zanzibar zimeweza kuungana kwa miaka 50, hakuna sababu ya Shirikisho la EAC kushindikana.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais Yoweri Mseveni wa Uganda, makamu wa kwanza wa rais wa Burundi, Prosper Bozombaza na waziri mkuu wa Rwanda, Dk Pierre Habumuremy.
“Nachukua fursa hii kwa niaba ya viongozi wenzangu kuwapongeza Rais Kikwete na Watanzania wote kwa kudumisha Muungano wao ambao ni wa kipekee kwa  bara la Afrika,” alisema Rais Kenyetta.
Kiongozi huyo aliwataka Watanzania kuulinda na kuudumisha Muungano huo ambao ni darasa la namna ya kuungana wakati huu wa mchakato wa kuanzisha shirikisho la kisiasa la nchi za Afrika Mashariki.
Kwa sasa Tanzania iko kwenye mchakato wa kuandika Katiba mpya na suala la muundo wa Muungano ndio linaonekana kutawala mjadala huo kutokana na baadhi ya watu kutaka muundo ubadilike na kuwa wa serikali tatu, huku kundi linaloongoizwa na chama tawala, CCM likitaka kudumisha muundo wa serikali mbili ulioboreshwa.
CHANZO, MWANANCHI




No comments:

Post a Comment