Pages

Pages

Pages

Saturday 3 May 2014

MRISHO AWALIZA WANAHABARI ARUSHA

Uzinduzi wa wimbo maalum wa wanahabari uliotungwa na kuimbwa na bendi ya Mpoto, inayoongozwa na Mrisho Mpoto, umewaliza baadhi ya wanahabari wanaohudhuria Kilele cha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani kwenye ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Wimbo huo, ambao umo pia katika albamu ya pili ya Mrisho Mpoto iitwayo 'Waite', ambayo nayo ilizinduliwa, umesheheni ujumbe maridhawa kuhusu madhira na madhara yanayowapata wanahabari nchini, huku akitolea mfano matukio ya kuuawa kwa Daudi Mwangosi, kuvamiwa kwa Saed Kubenea, Absalom Kibanda, Shaaban Matutu na wengineo waliowahi kupata madhira hayo.
Uzinduzi huo umefanywa na mgeni rasmi, Jaji (mstaafu) Mark Bomani.
Bado mambo yanaendelea hapa Arusha.

No comments:

Post a Comment