Muda wa maswali: Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alifanya mahojiano ya Q&A kupitia akaunti ya twita ya Yahoo Sport siku ya ijumaa.JOSE Mourinho amesema kuwa atawapa nafasi wachezaji vijana katika kikosi chake cha kwanza muda muafaka utakapowadia.
Kikosi cha vijana cha Chelsea kilishinda kombe la FA kwa vijana kwa mara ya tatu ndani ya miaka mitano baada ya kuwafunga Fulham mabao 7-6 kwenye mechi mbili mapema mwezi huu, lakini wachezaji wengi wa kikosi hicho cha vijana wameshindwa kuingia kikosi cha kwanza cha Mourinho.
Alipolizwa kama vijana wake wenye mafanikio wataingizwa kikosi cha kwanza, Mourinho katika mahojiano ya maswali na majibu, Q & A kwa njia ya Twita na mtandao wa michezowa Yahoo, alijibu kuwa; “Nawahitaji kwa muda muafaka. Sitaki waingie halafu wasifanikiwe”.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment