Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 16 May 2014

MISS UNI COLLEGE TEMEKE JUMAMOSI DAR LIVE, SNURA KULITEKA JUKWAA

1 (15)Mratibu wa mashindano ya Miss Uni-College Temeke, Silas Michael (katikati) akiwatambulisha baadhi ya warembo ambao Jumamosi watapanda jukwaani kwenye ukumbi wa Dar Live kuwania nafasi ya mshindi wa kwanza. Mashindano hayo yatapambwa na burudani kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Snura Mushi “Mamaa Majanga” .
Na Mwandishi Wetu
Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Snura Mushi “Mamaa Majanga” atapamba mashindano ya Miss Uni-College Temeke 2014 yaliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Dar Live Mbagala Jumamosi.
Mbali ya Snura ambaye atafanya shoo kwa kutumbuiza nyimbo zake zote kwa mara ya kwanza, pia bingwa wa masindano ya Tikisa dance 2012 Hassan Jigoro naye atapamba mashindano hayo yatakayoshirikisha juma ya warembo 12 kutoka vyuo mbali mbali vya elimu ya juu vilivyomo manispaa ya Temeke.
Warembo hao ni Martha Mashaka, Sarah Joseph, Diana Joachim Kato, Theola Benedict, Eliana Lucumay, Nyangeta Kuboja, Naila Haroun Yusuph, Martha Manzawa, Susan Joseph, Karen Swai, Sarah Jacob na Flora Kimaro.
Warembo hao wanatoka vyuo vya Kumbukumbu ya ya Mwalimu Mwalimu Nyerere, Chuo Cha Utalii, TIA na Magogoni. Mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh 300,000 na vocha ya manunuzi yenye thamani ya Sh250,000 kwenye dula la Robby One fashion,wakati mshindi wa pili atapata Sh250,000 na vocha ya manunuzi ya Sh250,000 na wa tatu Sh 200,000 na wanne na wa tano watapata sh100,000 kila mmoja.
Pia kutakuwa na zwadi ya kifuta jasho ya Sh50,000 kwa warembo waliobaki na zawadi ya simu tatu za Huwawei kwa warembo watakaoonyesha nidhamu ya hali ya juu, kujiamini na mrembo bora katika muonekano pichani.
Mashindano hayo yamedhaminiwa na Continental outdoor, Global Publishers, Robby One fashion, Clouds Media group, Leluu Saloon, New Habari Corporation,Mesho decoration, Millard Ayo, salut5, Huwawei , Lamada Hotel, Shamoo Hotel.

 CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment