Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 4 May 2014

MATUKIO MBALIMBALI YA HABARIPICHA KUTOKA BENKI YA NBC

photo3
photo1
photo2
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Industrial,  Judith Motta, (kulia) akiwafundisha kusoma baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in the Sun  ikiwa ni sehemu ya mpango wa mameneja wa benki hiyo kanda ya Dar es Salaam hivi karibuni kujitolea muda wao kufundisha kwenye vituo mbalimbali vya watoto  wanaoishi katika vituo vya watoto wenye mahitaji.  Wanafunzi wapatao 27 katika kituo hiki kinachokusanya watoto toka mitaani na kuwalea chini ya uangalizi wenye maadili mzuri na mafunzo ya kazi za mikono hawajui kusoma wala kuandika.
 
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo  cha Child in the Sun kilichopo  Mbezi Makabe wakifanya mazoezi ya kusoma na kuandika baada ya kutoka madarasani walikkofundishwa na timu ya Mameneja wa matawi ya NBC yaliyoko Kanda ya Dar Salaam. Tathmini ya wiki ya tatu inaonyesha watoto wote wameshajua kusoma na kuandika na changamoto inayofuata ni kuunganisha maneno na kutunga tungo zenye kuleta maana.



CHANZO FULL SHANGWE


No comments:

Post a Comment