Pages

Pages

Pages

Monday 12 May 2014

MAPACHA WAZALIWA WAKISHIKANA MIKONO


Mama wa mapcha hawa amesema mapacha wake ni zawadi kubwa kwake

Mama mmoja nchini Marekani, amejifungua mapacha waliozaliwa wakiwa wameshikana mikono.
Watoto hao pia walikuwa wanapumua bila usaidizi wowote walipotolewa kutoka katika mashine yenye hewa ya Oxygen.


Mama wa watoto hao, alisema kuwa watoto hao waliopewa majina ya Jillian na Jenna Thistlewaite walikuwa wameshikana katika kitovu na kutumia Kondo la nyuma moja , hali ambayo madaktari walisema ni ya kipekee.

"Tayari ni marafiki ,’’ alisema mama yao Sarah Thistlethwaite.

Walizaliwa Ijumaa katika jimbo la Ohio, wakiwa wameshikana mikono.

Inaarifiwa ni mama mmoja tu kati ya akina mama elfu kumi mwenye uwezo wa kujifungua mapacha wa aina hiyo.

Bi Thistlewaite, mwenye umri wa miaka 32,alilazimika kupumzika kwa wiki kadhaa kabla ya kujifungua kwani mapacha wanaozaliwa wakiwa wameshikana mikoni ni hali nadra ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya watoto hao kabla ya kuzaliwa.

Mama huyo alisema kupokea watoto wake ilikuwa zawadi tosha kwake wakati huu wa kusherehekea siku ya akina mama duniani.

CHANZO, BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment