Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 21 May 2014

DK. SHEN ATEMBELEA BANDARI YA ZANZIBAR

DSC_2644Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhamed Shein akifuatana na viongozi wa Wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano wakiingia lango kuu la Bandari ya Zanzibar iliyop Mlindi alipotembelea bandari hiyo.
DSC_2626Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhamed Shein akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Affan Othman Maalim (alievaa suti bluu na kofia) baada ya kutembelea ghala lililokuwa likitumika  kuhifadhia pembejeo za kilimo alipotembelea bandari  hiyo.
DSC_2731Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Muhamed Shein akifuatana   na viongozi wa Shirika la Bandari  Zanzibar kuangalia utendaji wa kazi katika bandari hiyo ambayo hivi sasa meli kubwa ya makontena  zinafunga gati na kushusha  mizigo kwa wepesi.
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                20 Mei , 2014
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali imelitaka Shirika la Bandari kuchukua hatua za haraka kushughulikia tatizo la msongamano wa makontena katika Bandari ya Malindi ili shughuli za bandari hiyo ziweze kufanyika kwa ufanisi.
Akizungumza mara baada ya kutembelea bandari hiyo pamoja na eneo linalohifadhia makontena matupu karibu na hoteli ya Bwawani wilaya ya mjini Unguja, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alisema kwa ujumla hali hairidhishi katika bandari hiyo kutokana na msongomano wa makontena.

“Bandari haina nafasi ya kuweka makontena yote yanayoingia na yanayotoka. Hali hainiridhishi mimi na kila mtu hapa. Kwa mfano leo hii bandarini kuna meli inashusha makontena karibu 350 mengine yakijazana kila mahala mpaka hapa Bwawani” Dk. Shein alifafanua.
Alijibu swali kuhusu madhumuni ya ziara hiyo alisema ilikuwa ni kuona maeneo yote ya bandari yakiwemo ya kuwekea makontena na pamoja na maghala mbalimbali ili kuona kipi kinaweza kufanyika kupata eneo kwa ajili ya kuondoa tatizo la msongomano wa makontena katika bandari hiyo.
Aliukumbusha uongozi wa Shirika hilo kuwa sehemu ya kuwekea makontena la Bwawani ni ya muda tu kama ilivyokubaliwa wakati wa uongozi uliopita wa Shirika hilo ulipokabidhiwa eneo hilo hivyo ana hakikika kuwa tangu wakati huo walikuwa wanafanya mipango mbadala wa kupata eneo jingine.
Alifafanua kuwa eneo hilo limo katika mpango wa Serikali wa uwekezaji kwa shughuli nyingine za maendeleo ambapo wakati wo wote linaweza kuchukuliwa kwa shughuli hizo hivyo uongozi wa bandari hauna budi kuzingatia hilo kwa kuharakisha mipango yake ya kuondoka katika eneo hilo.
Hata hivyo Dk. Shein alikiri kuwa Bandari ya Malindi hivi sasa imeshakuwa ndogo na itakuwa vigumu kukidhi mahitaji ya matumizi ya sasa ya bandari hasa baada ya mfumo wa usafirishaji wa bidhaa kubadilika kuwa wa kutumia makontena.
Kwa hiyo alieleza kuwa ndio maana jitihada za Serikali zimeelekezwa katika kutekeleza mpango wake wa ujenzi wa bandari mpya na ya kisasa huko katika eneo la Mpigaduru liliko kilomita chache kutoka bandari ya sasa ya Malindi.
Katika ziara hiyo Dk. Shein amelitaka Shirika hilo kuangalia upya matumizi bora ya baadhi ya majengo yake kwa kuyajenga upya ili kupata ofisi za kisasa na bora ili Shirika liweze kutoa huduma vizuri kwa wateja wake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Bwana Abdalla Juma Abdalla alisema lengo la kuhifadhi makontena matupu katika eneo la Bwawani ni kutoa nafasi kwa makontena yenye bidhaa kuweza kushushwa kutoka melini na kuokoa gharama na usumbufu pindi makontena hayo yakichelewa kushushwa kutoka melini.
Alibainisha kuwa Shirika lake inalipa kipaumbele suala la kuondosha msongomano wa makontena bandarini hapo na kwamba uongozi wa bandari wakati wote umekuwa ukihakikisha kunakuwepo na ufanisi katika utendaji wake. 
Katika ziara hiyo Dk. Shein alifuatana na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Wizara ya Kilimo na Maliasili pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis.
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment