Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 5 May 2014

CHELSEA YASUBIRI MIUJIZA KUTWAA UBINGWA, YAKAZIWA NA NOWRICH, ARSENAL MWENDO MDUNDO UEFA


 Doubt: Eden Hazard was fouled in the Norwich box but the referee blew for offside

CHELSEA imeshindwa kupanda kileleni katika msimamo wa ligi kuu soka nchini England baada ya kutoka suluhu pacha ya bila kufungana na Nowrich City.

Kwa matokeo ya leo, Mourinho anabakia katika nafasi ya tatu akiwa na pointi 79 baada ya kucheza mechi 37.

Kama Chelsea wangeshinda leo wangefikisha pointi 81 kileleni, huku wakisubiri matokoe ya mechi ya kesho kati ya Liverpool dhidi ya Crystal Palace.

Ili kutwaa ubingwa, Chelsea wanasubiri maajabu ya soka kutokea kwasababu wanaomba Man City na Liverpool wapoteze mechi zao zote za mwisho na wao kushinda mechi yao.
 Disbelief: John Terry reacts to Neil Swarbrick's decision to blow his whistle for offside

Kama Liverpool na Man City watapoteza mechi zote, halafa Mourinho akashinda basi atakaa kileleni kwa pointi 82.

Lakini kwa kiwango cha Man City na Liverpool kupoteza mechi zote yatakuwa ni maajabu makubwa katika ulimwengu wa soka.

Man city wapo kileleni kwa pointi 80 kufuatia ushindi wa mabao 3-2 waliopata jana dhidi ya Everton katika dimba la Goodison Park.

Liverpool wapo nafasi ya pili kwa pointi 80, lakini wanazidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Ili kutwaa ubingwa, Liverpool waliocheza mechi 36 sawa na Man City wanahitaji kushinda mechi zote mbili huku wakiombea Man City ashinde mechi moja na kutoa sare moja.

Kama Man City na Liverpool watashinda mechi zao zote za mwisho, bingwa atapatikana na kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, lakini Man City watakuwa wapo sehemu nzuri.

Mpaka sasa, Liverpool wamefunga mabao 96 na kufungwa mabao 46, ukitoa mabao ya kufunga na kufungwa unapata mabao +50.

Man City wamefunga mabao 96 na kufungwa 37, ukitoa mabao ya kufunga na kufungwa unapata +59.

Kwa hesabu hizo, Liverpool atahitaji kushinda mechi zake zote kwa mabao mengi zaidi ili kufuta tofauti ya mabao 9.
 article-2620048-1D9180BF00000578-38_634x361

Katika mechi nyingine, bao pekee la Mfaransa Olvier Giroud limewapa ushindi wa bao 1-0 Arsenal dhidi ya West Ham.
Kwa matokeo hayo, Asernal wamejihakikisha kumaliza nafasi ya nne na kufuzu UEFA mwakani.

CHANZO MPENJA BLOG


No comments:

Post a Comment