Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 18 May 2014

CCM WAVUNA WANACHAMA WAPYA ARUSHA


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

CHAMA cha mapinduzi CCM, Wilaya ya Arusha, jana kimevuna wanachama wapya  100 katika kata ya Unga limited wakiwemo waliokuwa viongozi wa Chadema hicho ngazi ya kata ambao ni Swalehe Fidua, aliyekuwa mwenyekiti na JJ Obuya ,aliyekuwa katibu kata.
Tukio hilo limetokea kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi katika kata ya Unga limited ,kutokana na hatua ya ziara  ya Kamati ya siasa ya wilaya kuhamasisha uhai wa chama cha mapinduzi ngazi ya kata na tawi.
Katika mkutano huo Chama cha Mapinduzi kimekomba wanachama hao 100 wakiwemo waendesha Boda boda ,ambao walikuwa wamefungua vijiwe vya Chadema katika maeneo ya Tindiga ambao wamelitelekeza tawi lao na kuhamia Chama cha Mapinduzi.
Mbali na kukomba wanachama hao pia Chama cha Mapinduzi kilifungua tawi jipya la Wakereketwa lililopo eneo la Esso, na kuifanya kata hiyo kuwa na matawi matatu, mengine ni Tindiga na Viwandani.
Mwenyekiti wa CCM, wilaya ya Arusha, Dakta Wilfred Soileri, amesema Chama cha mapinduzi kipo katika ziara ya kukagua Uhai wa chama ambapo kinatembelea kata zote na kufanya vikao vya ndani kisha mikutano ya hadhara ili kuelezea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
Ameongeza kuwa tayari kamati ya siasa ya wilaya imemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela, kufuatilia  ujenzi wa kituo kidogo cha polisi katika kata ya Sokoni one ambacho kimekwama tangia mwaka 1998 kilijengwa kwa nguvu za wananchi hadi leo hakijakamilika na hivyo kuwakosesha wananchi huduma ya ulinzi.
Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha, Kimaro, amesema kuwa  hivi sasa Chama kipo katika hatua ya kuimarisha uhai ngazi ya matawi na kata ambako ndiko kuna wanachama wa CCM, na kuendelea kunadi sera za CCM.
Kimaro, amesema kuwa Chama cha mapinduzi kina sera imara na madhubuti na hivyo zinawavutia wengi na ndio maana  wengi wameamua kujiunga na CCM, kutoka kwenye vyama vingine vya kisiasa ambavyo havina mwelekeo.
Amesema Chama cha Mapinduzi ni chama Imara na ndio chenye jukumu la kuongoza nchi, wanaorejea CCM, kutoka upinzani baada ya kuchoshwa na mambo waliyoyakuta huko na yamekuwa rtofauti na matarajio yao .
Amesema mbali na kuimarisha uhai wa Chama pia ziara hiyo inatumika kukutanisha wanachama ambao walikuwa hawaelewani na kusababisha mpasuko ambao unakipotezea ushindi chama cha mapinduzi katika chaguzi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment