Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 26 May 2014

BRENDAN ROGERS ASAINI MKATABA MPYA LIVERPOOL, AJIFUNGA MPAKA 2018

 BRENDAN Rodgers amepewa ofa nzuri ya kazi katika klabu ya Liverpool kwa kusaini mkataba mwingine utakaomfanya akae muda mrefu zaidi Anfield.
Rodgers, aliyebakiwa na miezi 12 katika klabu hiyo amepewa zawadi hiyo ya mkataba baada ya kufanya vizuri ligi kuu na sasa amemwaga wino katika mkataba mpya unaosemekana kumuweka  Merseyside mpaka  2018.
Liverpool walimaliza pointi mbili tu nyuma ya mabingwa Man City tangu mwaka 1990 na walionesha kiwango kikubwa mno chini ya Rodgers na kuwavutia Wamiliki wa klabu hiyo,  raia wa Marekani.
Tangu Rodgers ajiunge na Liverpool 2012 akitokea Swansea City amekuwa kivutio kwa mashabiki na wamiliki wa klabu hiyo na sasa wanajiandaa kumpa dau la kutosha kufanya usajili kwa ajili ya msimu ujao na michuano ya UEFA.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment