Pages

Pages

Pages

Tuesday 13 May 2014

AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI

DSC00207
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 13.05.2014.
  • MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI  KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI.
  • JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI.
  • JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUKUTWA NA BHANGI.
TUKIO LA KWANZA.
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA  KITWANA  S/O  LUGOYA  [30] MKAZI WA ILEMI-JUHUDI ALIUAWA  KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE  NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI  MAWE, FIMBO NA MARUNGU. CHANZO NI TUHUMA ZA UNYANG’ANYI/KUTEKA GARI. AWALI TAREHE 12.05.2014 MAJIRA YA  SAA 02:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MSHANGAMWELU, KATA YA  MSHEWE, TARAFA YA  BONDE LA USONGWE WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. STEPHEN S/O MGOGO [40] MKAZI WA KABALE AKIWA NA WENZAKE KWENYE GARI AINA YA  FUSO WALIKUTA MAWE YAMEPANGWA BARABARA YA MBALIZI/MKWAJUNI NA DEREVA  ALIPOSHUKA ILI KUTOA MAWE HAYO LILITOKEA  KUNDI LA WATU WANNE KUTOKA VICHAKANI  WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA NA MARUNGU WALIWAVAMIA NA KUWASHAMBULIA KISHA KUWAPORA PESA, SIMU ZA MKONONI NA PIKIPIKI MOJA T.682 CHT AINA YA  SANYA ILIYOKUWA NDANI YA  GARI HILO  NA KUTOWEKA KUSIKOJULIKANA. THAMANI HALISI YA  MALI ILIYOPORWA BADO KUJULIKANA. KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA PIKIPIKI  IMEPATIKANA NA WATUHUMIWA WAWILI 1. NDAYOBI  S/O LUTEGO  [26] MKAZI WA IGUNGA-TABORA NA 2. IDDI S/O  SADICK  [29] MKAZI WA VETA WAMEKAMATWA. MHANGA STEPHEN S/O MGOGO AMELAZWA HOSPITALI TEULE YA  IFISI HALI YAKE INAENDELEA VIZURI. 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI WANAPOWAKAMATA WATUHUMIWA KWA TUHUMA MBALIMBALI BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ICHUKULIWE.  AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA ALIYEKIMBIA  AZITOE  KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. PIA KAMADA MSANGI ANATOA RAI KWA JAMII HUSUSANI WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA WA MAZAO KUEPUKA TABIA YA  KUTEMBEA/KUWEKA NDANI YA  NYUMBA   KIASI KIKUBWA CHA FEDHA  ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA MSAKO.
JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI  KATIKA TUKIO HILO  JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA NAYORAMU S/O WAJEKAJE [42] MKAZI WA KIJIJI CHA MKWANGU NA MAJIGITA  S/O  MUSSA [40] MKAZI WA UVINZA MKOANI KIGOMA   BAADA YA  KUKAMATWA WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI NYAMA YA  MNYAMA INSHA YENYE UZITO WA KILO 3 PAMOJA NA NGOZI YA  KICHWANI YA  MNYAMA HUYO.
 WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA  TAREHE 12.05.2014 MAJIRA YA  SAA 15:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KISUNGU-MKWANGU, KATA YA  MAMBA,TARAFA YA  KIWANJA WATUHUMIWA NI MTUMIAJI NI WAWINDAJI HARAMU NA  TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA PILI JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAMSHIKILIA             
NAYORAMU S/O WAJEKAJE [42]  MKAZI WA KIJIJI CHA MKWANGU WILAYA YA  CHUNYA  BAADA YA  KUKAMATWA AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAMU 500.  
MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA  TAREHE  12.05.2014 MAJIRA YA  SAA 16:30HRS  HUKO KATIKA KIJIJI CHA MKWANGU, KATA YA  MAMBA,TARAFA YA  KIWANJA WILAYA YA  CHUNYA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI KUMFIKISHA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA  JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI  YA  DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA  ANATOA WITO KWA  JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA UWINDAJI HARAMU  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA, BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZILIZOPO KWA MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI.
                                                    Imetolelewa na:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
CHANZO FULL SHANGWE BLOG

No comments:

Post a Comment