Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 16 April 2014

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA DHANA YA KUJITAMBUA

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot.com

Walimu nchini kote wametakiwa kuwafundisha wanafunzi wao dhana ya kujitambua na kujiamini ili kuweza kushindana katika masomo yao na katika kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi vyuo hali ambayo itawasaidia kuweza kushuindana katika sekta ya elimu na ajira ndani na nje ya nchi na kuongeza ufaulu katika masomo yao.
Hayo yameelezwa jana na mkuu wa wilaya ya Arusha Bw.John Mongela wakatiakihutubia kama mgen rasmi kwenye mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule ya sekondari ya Mt,Theresia wa mtoto yesu ambapo iko chini ya Kanisa ya katoliki jimbo la Arusha iko iliyopo kata ya kisongo wilayan monduli katika Mkoa wa Arusha.
Hata hivyo alisema kuwa wanafunzi wengi anaohitimu masomo yao wengi wao hawajiamini wala kujitambua hali inayowafanya kutokufanya vizuri katikamasomio yao na hata wakipewa mahojiano ya kazi hawawezi kujielezea hata kwa dakikachache hali ambayo inawakwamisha katika jitihada zao za kimaendeleo na kujikwamua katika lindi la umaskini,
Aidha Mkuu huyo Mongela aliwataka wazazi washirikiane na walimu katika kuhakikisha suala la nidhamu linasimamiwa kwakaribu ambapo nidhamu ndio kila kitu katika maisha na mafanikio yao ya kilasiku ambapo hivi sasa nidhamu imeshuka kwawanafunzi walio wengi hali ambayo inawakwamisha katika masomo yao.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa shule ya sekondari ya Mt,theresia ya mtoto yesu Sista Mamelta Kibena alisema kuwa mbali na mafanikio ya kuanzishwa kwa shule hiyo miaka mitano iliyopita na kuwa na wanafunzi 593 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita bado wanakabiliwa nma changamoto mbal mbali ikiwemo ukosefu wa maktaba kubwa ya kuweza kmudu wanafunzi hao kwa wakati mmoja.
Hata hivyo mkuu huyo alitaja changamoto nyingine kuwa ni upungufu wa vifaa vya maabara, upungufu wa vyumba vya madarasa ambapo changamoto hizi zimekuwa kikwazo cha maendeleo ya kuweza kupambana na adui ujinga hivyo amewataka wadau wa eimu kwa kushirikiana na wazazi waweze kuwasaidia kutatua ili kuweza kuinua sekta ya elimu nchini.
Hata hivyo alisema kuwa shule yake imefanya vizuri katika mtihani wa mock wa mwaka 2014 ambapo kikanda wamekuwa wa kwanza  ambapo nawanafunzi hao wamefaulu kuanziadaraja la kwana hadi la tatu tu na walikuwa wanafunzi 35 tu na hali hiyo imesababisha na nidhamu nzuri na maadili mema wanayofundisha kwenye shule yao na miundombinu bora na mazingira mazuri ya kujisomea . 
Pia aliwataka wanafunzi kuwa waaaminifu na wawajibikaji ili kuwa na dira ya mafanikio katikamaisha yao ya shule na hata baada ya kuhitimu masomo yao ya kidato cha sita.

No comments:

Post a Comment