Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 1 May 2014

TUCTA IMEITAKA SERIKALI KUTOKA TAMKO KUHUSU MUSTAKABALI WA ELIMU NCHINI

Nicholaus-Mgaya

Katibu mkuu wa Tucta Bw. Nicolous Mgaya (Kushoto) akitoa hoja mbele ya waandishi wa habari

Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania(Tucta)limeitaka serikali kutoka tamko kuhusu mustakabali wa elimu nchini baada ya kujitokeza kwa kauli mbili tofauti zinazowachanganya wananchi
Akizungumza Jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu wa Tucta,Nicolaus Mgaya alisema kuwa, kujitokeza kwa kauli hizo mbili tofauti kunaonyesha wazi kuwa, serikali imeshindwa kujipanga wakati wa kutekeleza majukumu yake, jambo ambalo linawafanya kutoa kauli zinazokinzana.
“Kitendo cha serikali kutoa kauli mbili tofauti katika suala nyeti la elimu kunaonyesha wazi kuwa wameshindwa kujipanga,hivyo basi wanaweza kuiangamiza elimu kwa vijana wetu,”alisema Mgaya.
Alisema kuwa, hali ya elimu nchini ni mbaya ikilinganishwa na kipindi kilichopita,jambo ambalo linasababisha kuongezeka kwa idadi ya wananchi wanaoshindwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho.
Alisema kuwa,hakuna nchi yoyote duniani ambayo itatoa matokeo ya mwisho ya wananchi bila ya kuwepo kwa waliofaulu na waliofeli,kwa sababu matokeo hayo yanaleta changamoto kwa wanafunzi waliofanya vibaya kujituma zaidi ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani inayofuata.
Kwa mujibu wa Mgaya,kutokana na hali hiyo, serikali ilipaswa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wa elimu ili kujadili mustakabali wa elimu,hasa katika Nyanja ya walipotoka na waendako, jambo ambalo lingeweza kusaidia kupata maoni ambayo yanatoweza kuboreshwa na kuleta mabadiliko katika sekta hiyo.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo, maoni hayo wangeweza kuwa mwongozo mpya ambao ukitumiwa vizuri utaweza kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo,wananchi wangeweza kuona utofauti wa hali halisi ya elimu kwa vijana wao,jambo ambalo lingeweza kuleta maendeleo.
Alisema kuwa, kutokana na hali hiyo, wanapaswa kujifunza kwa yale yaliyotokea na kuanza mchakato wa kushirikisha wadau ili waweze kuleta mapinduzi katika sekta ya elimu ambayo itasaidia uboreshaji wake katika Nyanja mbalimbali ya sekta hiyo.
CHANZO, PT BLOG

No comments:

Post a Comment