Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 23 April 2014

TANZANIA IKIZALISHA VEMA NJAA ITAONDOKA

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot.com, Arusha

IMEELEZWA kuwa ili nchi ya Tanzania iweze kuepukana na majanga  hasa ya baa la njaa Nchi inapaswa kuzalisha kilimo kwa asilimia zaidi ya sita ambapo chakula kinachozalishwa kitaweza kuwekwa hadi akiba tofauti na sasa ambapo uzalishaji wa kilimo ni kwa asilimia 4 pekee.
Hata hivyo, uzalishaji huo wa asilimia sita pia utaweza kuongeza ufanisi wa kilimo na kitakuwa ni cha kisasa zaidi hivyo majnga hasa ukosefu wa chakula,umaskini nao utaweza kupungua kwa kiwango kikubwa sana.
Hayo yameelezwa na Bi Nkuvililwa Simkanga ambaye ni mkurugenzi wa sera na mipango kutoka katika Wizara ya kilimo na ushirikia wakati akiongea kwa niaba ya wizara hiyo mara baada ya kukabidhiwa kwa Jengo la kuhifadhia mazao ambalo limejengwa chini ya uzamini wa  TAHA.
Mkurugenzi huyo alidai kuwa kwa sasa Tanzania bado inazalisha Kilimo kwa kiwango cha Asilimia 4 pekee hali ambayo bado inahitajika kuongezewa nguvu zaidi kwani uwezekano wa kuendelea kuzalisha kwa wingi sana bado upo endapo kama kutakuwa na umoja baina ya wakulima na wadai wengine wa Kilimo.
"Tukizalisha kilimo chenye ubora na kiwango ambacho kinahitajika basi tutaweza kupunguza tatizo la uhaba wa chakula na hata umaskini nao utapungua kwani uwezo wa kufanya hivyo tunao kabisa ila changamoto bado zinashindwa kutufikisha"aliongeza Bi Simkanga.
Mbali na hayo alisema kuwa Kilimo kinachangia uti wa mgongo wa taifa kwa asilimia 24.7 huku wananchi nao wakiwa wanategemea kama ajira kwa asilimia 75 ambapo pia asilimia 95 ya chakula kinachotumika hapa nchini kinatokana na kilimo.
"Takwimu zinaonesha kuwa hali si mbaya sana na kilimo kinaendelea vizuri sana ingawaje pia wakulima wana uwezo mkubwa sana wa kuzalisha chakula kingi na hata kikaweza kupelekwa nje ya nchi hivyo jitiada za makusudi zinahitajika kwa haraka sana," aliongeza.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa TAHA Erick Ngmario    erick alisema kuwa ili wakulima waweze kufikia malengo yao ya kila siku wanatakiwa kuachana na mila ambazo zimepitwa na wakati kwani wakati mwingine zinasababisha waweze kulima kilimo cha umaskini.
Erick alidai kuwa moja ya mila hizo amnazo zimepitwa na wakati ni pamoja na mila za kulima kwa mazoea bila kulima kilimo cha kisasa hali ambayo wakati mwingine husababisha umaskini ingawaje wanatumikia Kilimo kila mara. 
"kwa sasa wakulima wanatakiwa kujifunza kulima kilimo ambacho kinatija na kamwe wasikubali kulima ili waweze kuonekana kama wamelima bali sheria, taratibu na mbinu za kilimo zinaitajika kufuatwa"aliongeza Erick.
Alimalizia pia kwa kuwataka wakulima hasa wa Eneo hilo la Midawi wahakikishe kuwa wanatumia vyema jengo hilo kwa ajili ya kuhifadhi mazao na kisha kuondokana na changamoto ya kuharibika kwa mazao.

No comments:

Post a Comment