JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAHADHARI NA MTANDAO WA UTAPELI UNAOJIITA TCRA FOUNDATION
Mamlaka ya Mawasiliano imebaini kuwa
kuna mtandao wa matapeli wanaotumia jina la Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) kwa kutumia tovuti inayojiita “TCRA Foundation” na
inayodanganya kutoa mikopo kwa maendeleo kwa watu.
Tovuti inayotumika ni http://tcra-foundation.wix. com/tcrafoundation
Mtandao
huu umetengenezwa wa kutumia picha zilizopo kwenye mitandao mbalimbali
zikiwaonyesha Raisi Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Makawe Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Prof. John Nkoma.
Aidha
mtandao huu unadai kuwa Mamlaka kwa kushirikiana na Kampuni za Simu za
Vodacom na Tigo pamoja na Benki ya CRDB na NMB zinashirikiana kuendesha
Foundation hiyo.
Mamlaka ya Mawasiliano inawatahadharisha wananchi
kuwa haina “Foundation” yoyote ya kutoa misaada ya fedha. Mtandao huu
unatumika kuwalaghai wananchi na kuwaibia fedha zao kwa kuwataka watume
fedha za kujiunga na mtandaqo huo kwa number za simu za Tigo na Vodacom
zinazoonesha kusajiliwa kwa jina la Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania. Sio kweli na ni wizi na udanganyifu.
Mamlaka ya Mawasiliano inawataka wananchi kuwa na
tahadhari na watu hawa ambao hutumia mitandao ya Mawasiliano ya simu na
intaneti kufanya utapeli. Usitume fedha wala kujiunga na mitandao ya
namna hii.
Aidha Mamlaka ya Mawasiliano inawaomba wananchi
kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa wanapobaini utapeli wa namna hii kwa
kutoa taarifa kwa Mamlaka kwa vyombo vingine vya usalama ikiwa watahisi
au kuwa na taarifa za watu wanaojihusisha na udanganyifu huu katika
mitandao ya Mawasiliano ili kuzuia vitendo hivi vilivyoshamiri katika
siku za hivi karibuni.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
8Aprili 2014
No comments:
Post a Comment