Pages

Pages

Pages

Saturday 8 February 2014

MRADI WA MAJI ULIOZINDULIWA NA JK 'CHOKA MBAYA'

 
 
 
 
 
 
Mradi wa maji Pawaga uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete Machi 21, 2012 uko taaban baada ya katika Jiwe la Msingi kukatika na wahusika kushindwa kuliunganisha.
Badala yake, bomba hilo limeunganishwa nje ya eneo husika ambako limepandishwa kwenye kinguzo kama linavyoonekana kwenye picha hizo.
Mradi huo ambao unahudumia vijiji nane vya Tarafa ya Pawaga kwa sasa, ulijengwa kwa ufadhili wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruaha kwa ushirikiano na Jumuiya ya Ulaya, Christian Engineers in Development, Tear Australia, na Tear Fund United Kingdom.

No comments:

Post a Comment