Pages

Pages

Pages

Friday 10 January 2014

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA



RPC wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi

Watu wawili wafariki dunia mkoani Iringa katika matukio mawili tofauti likiwemo la mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Nyamihuu mkoani Iringa kupata ajali ya trekta aliyokuwa akiendesha kuacha barabara na kupinduka.
Imedaiwa mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina Herman Sanga (22) alikuwa akiendesha trekta lenye namba za usajili 6656 aina ya Fiat mali ya Kriakos Kalogeresi mkazi wa Iringa alikuwa akitokea shambani akielekea nyumbani ambapo trekta alilokuwa akiendesha liliacha barabara na kupinduka  na kusababisha majeruhi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Januari 5.
Hata hivyo alisema kuwa majeruhi huyo alikimbizwa katika hospitali ya serikali Tosamaganga kwa matibabu zaidi ambapo majira ya saa mbili usiku alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu. Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mtuhumiwa mmoja aliyejulikana kwa jina la Denis Kamugisha (34) kwa kosa la kumgonga mwendesha pikipiki ambaye jina lake halijafahamika na kusababisha kifo kwa abiria wake aitwaye Constantine Msuva mkazi wa Boma la Ng’ombe huku dereva wa pikipiki akiwa amelazwa na hawezi kuzungumza.
Kamanda Mungi alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 5, mwaka huu majira ya saa 9:50 alasiri maeneo ya Boma la Ng’ombe, Kata ya Dabaga, Tarafa ya Kilolo wilayani Kilolo ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akiendesha gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajiri T222APR alimgonga mwendesha pikipiki aina ya Sky Mark ambapo namba za usajiri hazijafahamika. Chanzo cha ajali bado hakijafahamika.
Aidha, Kamanda Mungi amesema mbali na matukio hayo mawili ya ajali, pia watu wasiofahamika waliiba ng’ombe kumi na tisa (19) wenye thamani ya TShs. 11 milioni mali ya Maganga Madagana (27) mkazi wa Kijiji cha Mfyome, ambapo watuhumiwa wanatafutwa.

No comments:

Post a Comment