Pages

Pages

Pages

Friday 10 January 2014

MKOA WA IRINGA WAJISIFU KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI MWAKA 2013


Wanahabari wakiwa katika  kikao hicho  leo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma  akizungumza na wanahabari leo juu ya utekelezaji wa Ilani  ya Uchaguzi kwa mwaka 2013.
Wanahabari wa vyombo mbali mbali wakifuatilia kikao cha  RC Iringa.
Wakuu wa idara wakiwa katika kikao cha Mkuu wa Mkoa na wanahabari leo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma kulia akieleza jinsi ambavyo mkoa ulivyotekeleza Ilani ya Uchaguzi kwa mwaka  2013.


SERIKALI ya Mkoa wa Iringa leo imetoa taarifa ya  utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa mwaka 2013 huku ikijivunia mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa.
Akitoa taarifa hiyo leo mbele ya wanahabari Mkuu  wa  Mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma alisema kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ambayo mkoa wa Iringa  unajivunia ni katika sekta ya elimu, miundo mbinu, kilimo, afya na nyingine nyingi.
Kwani alisema kuwa mkoa umepiga hatua katika ujenzi wa nyumba za walimu katika Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa, lengo likiwa kuendelea kuboresha kiwango cha elimu katika mkoa.
Akielezea kuhusu sekta ya afya alisema kuwa hadi sasa hospitali mbili zinaendelea kujengwa katika Manispaa na Kilolo, pia vituo vya afya na nyumba za watumishi wa afya ikiwa ni pamoja na kuendelea kusambaza dawa katika vituo vya afya.
Mkuu huyo wa mkoa alisema pia kumekuwepo na ufuatiliaji  wa huduma  zinazotolewa katika vituo hivyo na hospitali.

CHANZO: matukiodaima.com

No comments:

Post a Comment