Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 2 January 2014

LOWASSA: NIMEANZA SAFARI YENYE MATUMAINI


Na John Mhala, Monduli 

MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa amesema ameanza safari yake jana yenye matumaini makubwa kwa Watanzania, lakini yenye vikwazo vingi, ingawa anasema ana uhakika wa kufika na kushinda.
Lowassa alisema hayo jana katika Ibada ya shukurani yake na familia yake, kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Monduli mkoani Arusha.
Ibada hiyo ilikwenda sanjari na harambee ya ujenzi wa hosteli na zilipatikana zaidi ya Sh milioni 89. Lowassa alisema safari aliyoianza jana, ana uhakika wa kufika salama na kushinda; Ina matumaini makubwa kwa Watanzania kwa kuwa itakuwa na elimu bure, maji safi na salama, huduma za afya zenye uhakika lakini safari hiyo ina vikwazo.
Alisema atakapofika salama na kushinda katika safari hiyo, huduma hizo zitapatikana bila shaka yoyote. Alisema pamoja na miiba, mabonde na makorongo makubwa na milima, Bwana Yesu ni kiongozi katika safari hiyo, hivyo ana uhakika wa kufika na kushinda.
Alisema kila binadamu ana malengo katika maisha na hakuna asiyejua malengo yake katika maisha na ndoto zake.
"Nina malengo ya maisha yangu na malengo hayo hakuna asiyejua na nina faraja kubwa na malengo na ndoto zangu, nina uhakika wa kufika katika safari ninayoanza na kushinda kwa kuwa mbele ya safari hiyo anaiongoza Bwana Yesu Kristo,’’ alisema bila ya kufafanua.
Akizungumzia Rasimu ya Katiba, Lowassa aliliomba Kanisa kuiombea ijadiliwe kwa amani na upendo.
Kaimu Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati, Mchungaji Solomon Massangwa aliomba Serikali kutoa ruzuku kwa shule za dini, kwa kuwa zina mchango mkubwa kwa jamii.
Mchungaji Massangwa alizungumzia pia suala la Serikali, kutoa dawa katika hospitali za dini kuwa utoaji unacheleshwa na kufanya hospitali hizo kukosa dawa kwa muda fulani.

CHANZO: Habarileo

No comments:

Post a Comment