Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 1 January 2014

HALELUYA! TUMEUONA 2014, MIAKA 28 TANGU BABA AFARIKI

Ndugu zangu,
Hatimaye tumeweza kuvuka mwaka 2013 na kuingia 2014. Siku zinaongezeka na umri unasonga. Ni jambo na kumshukuru Mungu kwa wema wake. Sisi siyo watakatifu kuliko hao wengine ambao walitamani kuiona siku hii, lakini ni kwa neema yake tu tumeweza kufika.
Nakumbuka miaka 28 iliyopita, majira kama haya ndipo nilipompoteza baba yangu mzazi, Mzee Mahelela Mbega, ambaye wakati huo alikuwa na miaka 103. Kwahiyo, pamoja na kusherehekea kuingia mwaka mpya, lakini nakumbuka kifo cha baba mpendwa.
Kimsingi, tusihuzunike kwa kushindwa kufanikiwa katika mipango yetu tuliyojiwekea mwaka 2013, bali tuangalie changamoto gani zimesababisha tusiyafikie.
Muda bado upo ingawa unasonga mbele, hivyo mwaka huu kila mtu lazima awe na malengo yake na ajitahidi kuhakikisha walau anayafikia kwa asilimia fulani.
Naamini kwa bidii, juhudi na maarifa pamoja na kumtegemea Mungu, kila kitu kinawezekana.
HERI YA MWAKA MPYA! BONNE ANNE 2014!

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Iringa

No comments:

Post a Comment