Kampuni moja ya kutengeneza majeneza nchini Poland imelikera kwa mara nyingine Kanisa Katoliki kutokana na kutumia wanamitindo wakiwa uchi ili kupromoti biashara hiyo ya majeneza.
Kampuni hiyo inayoitwa Lindner imechapisha kalenda yake ya mwaka 2015, ikiwa na maelezo makubwa ya 'UHUSIANO WA MWANAMKE NA MWANAMUME' (Male-Female Relations), lakini ikiwa na picha nyingi za rangi nyeusi na nyeupe.
Watengenezaji wake wanasema picha katika kalenda hizo zimelenga kuonyesha uimara, nguvu na unyoofu wa wanawake, na wakati huo huo kusaidia kuuza majeneza.
Picha ya mwezi Novemba kwenye kalenda hiyo, kwa mfano, inaonyesha mwanamke akiwa uchi akiwa amelala juu ya jeneza, huku mfuniko wake ukiwa umefunguka kidogo na mikono ya mwanamume ikiwa imeshikilia mfuniko huo na sehemu ya jeneza.
Picha ya mwezi Machi kwenye kalenda inaonyesha mwanamke aliye uchi akiwa amefungwa juu ya jeneza huku mkanda ukiwa umeshikiliwa na mwanamume.
Kalenda hiyo ni mpya katika mfululizo wa kampeni za aina hiyo zinazoanywa na kampuni hiyo ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele na Kanisa Katoliki nchini Poland kwamba 'hazifai'.
Msemaji wa kanisa hilo alisema kwamba vifo vya binadamu vinapaswa kuchukuliwa kwa umakini, unyenyekevu na heshima na kwamba havipaswi kuchanganywa na mapenzi.
Lakini mmiliki wa kampuni hiyo Zbigniew Lindner alisema: "Tulitaka kuonyesha kwamba jeneza halipaswi kuwa kitu cha kuogopwa - ni samani, ni kitandacha mwisho ambacho mtu atakilalia.
"Siyo alama ya kidini. Ni bidhaa. Kazi zetu nyingi zinakwenda kwenye majeneza ambayo huonwa kwa muda mfupi tu wakati wa maziko.
"Mtoto wangu alikuwa na mawazo ya kubuni kalenda ya kampuni ili tuweze kuonyesha kitu makini kidogo, kinachovutia, kizuri; uzuri wa wasichana wa Poland na uzuri wa majeneza yetu."
CREDIT: BROTHERDANNY BLOG NA MASHIRIKA

No comments:
Post a Comment