Pages

Pages

Pages

Saturday, 8 November 2014

HII NDIYO NDEGE YA KIJASUSI ILIYOTUA BAADA YA KUWA ANGANI KWA MIAKA MIWILI!


Ndege ya jeshi la Marekani iliyorushwa kwa siri angani imetua hivi karibuni huko California baada ya kuwepo katika anga za juu kwa muda wa siku 674 (miaka miwili).

Taarifa za kiintelijensia zinaeleza kwamba, ndege hiyo yenye muundo wa Boeing ikiwa na namba X-37B Space Plane ilirushwa angani na jeshi la anga la Marekani kwa usiri mkubwa sana na haijajulikana misheni yake ilikuwa nini.
Wapo wanaosema kwamba huenda ndege hiyo, ambayo inaweza kutua yenyewe, ilipelekwa angani kwa nia ya kukusanya taarifa za kijasusi kutoka katika mataifa mengine kwa kunasa taarifa hizo kutoka katika satelite.
Wengine wanasema, huenda ndege hiyo isiyo na mabawa, ililenga kuharibu satelite za mataifa hasimu na wengine wakisema yawezekana ilikuwa ikikusanya taarifa kutoka Mashariki ya Kati.
Angalia video kwa habari zaidi.

CREDIT: BROTHERDANNY BLOG NA MASHIRIKA

No comments:

Post a Comment