157 wameaga dunia katika mkasa wa moto ndani ya mgodi
Mlipuko katika mgodi wa
makaa ya mawe magharibi mwa Uturuki umesababisha vifo vya zaidi ya wachimbaji
migodi 200 na kujeruhi wengine wengi kujeruhiwa kwa mujibu wa maafisa nchini
humo.
Waziri
wa kawi, Taner Yildiz, amesema kuwa zaidi ya wafanyikazi 780 walikuwa katika
mgodi huo pale kuliposikika mlipuko katika kitengo cha kusambazia umeme.
Waokoaji
wanajaribu kila mbinu kuwafikia mamia ya wachimba migodi.
Inahofiwa
kuwa wachimbaji mgodi wengine wengi bado wamefukiwa chini ya mgodi huo.
Inakadiriwa
kuwa wakati mlipuko huo ulipotokea wafanyikazi 780 walikuwa ndani ya mgodi huo
japo inaaminika wengi waliweza kukimbilia usalama wao
.
Bado
idadi ya walionaswa ndani ya mgodi huo haijabainika.
Mgodi
huo uko katika mji wa Soma, mkoani Manisa , takriban kilomita 250 kusini mwa
Istanbul.
Jamaa
za wachimbaji migodi hao wamekusanyika katika makundi karibu na mgodi huo ambao
unamilikiwa na wawekezaji wa kibinafsi huku wengi wao wakilia hadharani na
kububujikwa na machozi.
Waziri
wa nishati Taner Yildiz ameimabia televisheni ya Uturuki kuwa huenda wengi
wamekufa kutokana na sumu ya gesi aina ya carbon monoxide.
Amesema
moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme.
Picha
za televisheni zinaonyesha maafisa wa uokoaji wakiokoa wafanyikazi wa mgodi
huo, huku nyuso zao zao zikiwa zimejaa vumbi.
Baadhi
yao wanaweza kutembea na wengine wanabebwa na kupelekwa ndani ya magari ya
kubebea wagonjwa yaliyoegezwa karibu na eneo la tukio.
CHANZO, BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment