Na Philemon Solomon wa Fullshangwe Dar es Salaam
Wito umetolewa kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kushuhudia shindano kubwa na la aina yake la kuwania taji la urimbwende linalotarajiwa kufanyika tarehe 21 juni 2014 katika ukumbi wa Mkonge hotel.
Akiongea na wana habari kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Nice and lovely Bi Rejina Gwae amesema kuwa wanajivunia kupata nafasi ya kuwa waandaji wa shindano hilo na kutoa wito kwa warembo wote wenye nia ya kushiriki kujitokeza kwa wingi.
Kuhusu zawadi kwa mshindi Bi Rejina amesema kuwa mshindi ataondoka na gari lenye thamani ya shilingi miliono 10 toka kwa kampuni ya Nice and lovely akasema kuwa pia kuna zawadi nyingine za pesa taslimu toka kwa washindi wengine ambazo wanatarajia kuzitangaza baadae.
Kwa upande wake meneja mauzo wa Loreal wamiliki wa bidhaa za Nice and lovely Briyan Kelly alianza kwa kuishukuru kampuni ya Mac D promotion kwa kuwapa nafasi ya kuwa wadhamini wa nafasi hiyo na kuahidi kuitendea haki nafasi hiyo.
Akamalizia kwa kutoa wito kwa wote wenye nia ya kushiriki katika shindano hilo kujitokeza kwa wingi na kusema kuwa fomu za kushiriki zinapatikana Mkonge hotel, D,boutique tanga mjini,Breez fm,Tanga beach resort, Five brothers, Mwambao fm, Sophia records, Danny fashion barabara ya 13, ofisi za the guardian tanga barabara ya 15 na Yolanda salon mtaa wa Eckenford na Nyumbani hotel.
CHANZO FULL
SHANGWE
No comments:
Post a Comment